Jose Chameleone ni mmoja wa wasanii tajika wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Huchomoa angalau kibao kimoja maarufu kila mwaka, jambo ambalo limemzidishia idadi ya mashabiki barani. Hata hivyo, msanii huyo kutoka Uganda anaithamini Kenya sana kuliko taifa lolote lingine Afrika.

Mwimbaji maarufu wa Uganda Joseph Mayanja, anayetambulika kama Jose Chameleone, ako na mvuto spesheli kwa Kenya na wananchi wake.

0fgjhs6etp0g9jnua-abe5068b

                                                        Jose Chameleon

Ni upendo mkuu kiasi kwamba wakati mmoja 2015 alitishia kugura taifa lake asili la Uganda na kuchukua uraia wa Kenya kwa kile alichosema ni upendo wa dhati wa Wakenya ikilinganishwa na Waganda.

Chameleone hutumia muda wake mwingine nchini Kenya akitumbuiza katika tamasha mbalimbali na kujumuika na wandani wake.

Muziki wake pia unafanya vyema nchini huku mashabiki wakimtambua kwa nyimbo stadi kuwaliko wasanii wengine.

Je, kwanini Chameleone anaipenda Kenya kiasi hicho?

Akizungumza na shirika la kupeperusha habari la DSTV, msanii huyo wa wimbo maarufu wa Tubonge alisema kuwa Kenya ilimuonyesha upendo alipokuwa katika dhiki hususan alipopewa makazi nchini na kumuwezesha kung’oa nanga taaluma yake ya muziki.

Katika mahojiano 2015, Chameleone alifichua jinsi aliingia nchini kimagendo kupitia gari la usafiri, na aliponaswa mjini Nairobi maafisa walikubali maelezo yake na kumruhusu kuanza maisha hapa.

Baadaye alirekodi wimbo wake wa kwanza kabisa Mama Mia ambao ulipokelewa vyema na kuibuka kuwa maarufu sana.0fgjhs7sgpieur6mt-798b340d

                                         Chameleone na Maina Kageni ni marafiki wa dhati

Chameleone ni rafiki wa karibu sana na mtangazaji Maina Kageni wa redio ya Classic 105. Wawili hao ni kama chanda na pete , mtangazaji huyo hajawahi kukosa kucheza wimbo wa Chameleone katika shoo yake ya kila asubuhi.

Msanii huyo wa Uganda asema anampenda Maina kwa sababu alikuwa mtangazaji wa kwanza wa redio kucheza wimbo wake wa Mama Mia nchini Kenya, nyakati hizoMaina akihudumu katika kituo cha Nation FM.

Msanii huyo ameshirikiano kutoa kibao na kikundi cha Kenya cha Elani – kinachojumuisha Maureen Kunga, Wambui Ngugi na Brian Chweya – ambacho majuzi kilisuta Chama cha Haki Nakili cha Kenya (MCSK) kwa kujaribu kuwaangamiza kimuziki kilipowanyima malipo yao ya usanii kinyume cha sheria.

Comments

comments