SHARE

[ad_1]

Diamond Platnumz aliamua kutosema chochote wakati alipokuwa Afrika Kusini kufanya video ya wimbo aliowashirikisha P-Square. Ni Paul na Peter Okoye tu ndio waliopost picha za behind the scenes za uchukuaji wa video hiyo.

Diamond

“Sometimes naonaga ukianza kuelezea kitu kitakuja, kitakuja, kinakuwa kinaboa,” Diamond ameiambia Bongo5.

“Sema tumeshamaliza tumeshashoot video, nasubiria tu mimi mwenyewe, nimekaa nayo tu ndani naangalia nitoe saa ngapi, imeshaisha kila kitu. Na muziki sometimes unafaa kuchungulia kuangalia unaiweka wapi, na kwasababu sio kutoa tu nyimbo unataka uonekana umefanya wimbo, lakini pia unatoa nyimbo kwa target za kibiashara,” ameongeza.

“Kwahiyo napotoa wimbo naangalia ni msimu gani niutoe ili nitengeneze pesa nyingi kuliko kuonekana tumefanya.”

Diamond amedai kuwa wakati wa kufanya video mapacha hao waliisimamia video kama yao na walionesha ushirikiano mkubwa. “Wamefanya video kutoka katika moyo wao kabisa kwasababu video zangu mimi zinakuwa zinahusisha kudance na vitu kama hivyo, so wakati party ya dance inakuja, Peter alisema ‘usijali, niachie hiki kitengo nakishika mimi hapa’ akawa anadeal na akina Mose Yobo. Paul akawa anasimamia sehemu za kuimba, kwahiyo wamefanya kwa mapenzi yao kabisa na hawakuwa wanaonesha kama watu wenye tatizo,” amesisitiza Diamond.

“It’s just maybe mwenyezi Mungu alipenda itokee kuwa watu walikuwa na matatizo halafu project ya kwanza kutoka ikatoka wakiwa na mimi, nafikiri itafanya vizuri zaidi.”

Hata hivyo Diamond amsema management yake ndiyo itakayoamua lini kazi hiyo itoke.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments