SHARE

[ad_1]

Mtayarishaji wa muziki wa Uprise Music Record, yenye maskani yake Mbagala jijini Dar es salaam, Duppy, amefunguka na kudai kwamba hali za maproducer wengi kiuchumi Tanzania ni mbaya ukilinganisha na wasanii wanaowatayarishia kazi zao.
10810085_715599991851048_738652080_n
Duppy (wa mbele katika picha) akiwa na baadhi ya wasanii

Akiongea na Times Fm, Duppy amedai biashara kwa upande wao si nzuri kwani wasanii wakubwa hawalipii vizuri kama wadogo.

“Mimi nafanya kazi kwa laki 7 nafikiri ndio nipo cheap ukilinganisha na wengine, sikufichi, marafiki zetu ni Underground wasanii wakubwa hawalipi pesa, ukiwatajia mkwanja ndio wanakukimbia kabisa” alisema Duppy.

Moja kati ya kazi ambazo amefanya Duppy ni wimbo’Headache’ wa Mabeste, ‘Walalahoi’ wa Izzo Biznez na nyingine nyingi za wasanii wakubwa.

Source:Times FM

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments