SHARE

Bendi ya muziki, Sauti Sol, haikuwatumbuiza mashabiki  katika uzinduzi wa chama cha Jubilee Party wala katika sherehe za kuadhimisha miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa chama cha ODM

Wanamuziki wa kikundi cha Sauti Sol waliwashangaza wengi walipokosa kutotumbuiza wafuasi wa Jubilee Party wakati wa uzinduzi wa chama hicho siku ya Jumamosi, Septemba 10.

Sauti Sol pia hawakuwa katika sherehe za kuadhimisha miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa chama cha ODM jijini Mombasa.

0fgjhs5vc139r237o-606ba41a

Bendi ya wanamuziki ,Sauti Sol

Kwa ukubwa wake humu inchini, ilitarajiwa labda kikundi hicho kingetumbuiza mashabiki wa chama ambacho kingewalipa pesa mingi.

Bien Aime ambaye ndiye kiongozi wa bendi hiyo alisema kuwa bendi hiyo haikuona umuhimu wa kuwatumbuiza wafuasi wa Jubilee Party wala wa chama cha ODM kwa sababu hakijihusishi na sherehe zozote za kisiasa.

0fgjhs7kvads28a0u-e35ef719

Sauti Sol haikuwatumbuiza mashabiki katika uzinduzi wa chama cha Jubilee Party wala katika sherehe za ODM.

“Wafuasi wangu wako katika vyama vote vya kisiasa. Hatujihusishi na siasi sisi,” akinukuliwa na Kenyans.co.ke

Aidha, Itumbi alitibithisha habari hiyo ya Bien na kusema kuwa kikundi hicho hakikualikwa katika utumbuizaji kwa hofu ya kuwapoteza wafuasi wao walio katika vyama tofauti vya kisiasa.

Comments

comments