SHARE

[ad_1]

Manchester United wanatarajia kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya, BBC Sport imeripoti.

image

Inaaminika kuwa deal hiyo na raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 ilikubaliwa kabla ya ushindi wa United kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.

Ikiwa United imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya chini ya kocha wake wa sasa, Louis van Gaal, uongozi wa Old Trafford unafikiriwa kuamua kufanya mabadiliko yanayohitajika.

Mourinho amekuwa benchi tangu atimuliwe na Chelsea December mwaka jana.

Klabu hiyo imepanga kutangaza ujio wake mapema wiki ijayo baada ya kumwambia Van Gaal, 64, afungashe virago vyake.

Kocha huyo raia wa Uholanzi bado ana msimu mmoja kwenye mkataba wake wa miaka mitatu na licha ya kutumia paundi milioni 250 kusajili wachezaji wapya, ukocha wake umewaangusha mashabiki wengi kwa timu yake kumaliza katika nafasi ya nne na kisha ya tano kwenye ligi kuu ya England katika misimu miwili aliyoifundisha.

Mourinho alikuwa kwenye mchezo wa masumbwi Jumamosi hii ambapo bondia David Haye alishinda lakini alikataa kuongea chochote iwapo anaenda kumrithi Van Gaal.

Mourinho ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi huku akishinda vikombe vitatu akiwa na Chelsea, pamoja na kuingoza  Porto na Inter Milan kwenye ushindi wa ligi ya mabingwa mwaka 2004 na 2010.

Aliwahi pia kuwa kocha wa Real Madrid na kuiwezesha kushinda kombe la Spanish La Liga mwaka 2012.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments