SHARE

[ad_1]

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu amejibu upya swali lililomponza bosi wake wa zamani, Charles Kitwanga.
swali+la+kitwanga

Uamuzi wa kurudia swali hilo ulitolewa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema swali hilo lilijibiwa katika hali ya ulevi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na wabunge wakaomba mwongozo kuhusu majibu yaliyotolewa.

Kitwanga aliondolewa katika nafasi yake na Rais John Magufuli baada ya kujibu ya swali hilo akiwa amelewa.

Leo, Masauni amejibu swali hilo namba 211 la Mbunge wa Viti Maalumu Devota Minja (Chadema) na kuonyesha utofauti mkubwa kati ya majibu yake na yale yaliyotolewa mwishoni mwa wiki na aliyekuwa Waziri wake.

Swali hilo ambalo awali lilikuwa namba 205, liliulizwa na Devota Minja akitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya polisi na askari magereza wanaoishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi ukilinganisha na kazi zao kwa jamii.

Nyakati zote hizo, swali hilo limeulizwa na wabunge tofauti wa Chadema kutokana na Minja kutokuwapo, mara ya kwanza likiulizwa na Suzan Kiwanga (Mlimba) na leo Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo.

Tofauti ya majibu ya Kitwanga, Masauni ametoa takwimu katika ujenzi wa nyumba 9,500 za Magereza nchi nzima, lakini kwa upande wa nyumba za Polisi majibu yalikuwa yaleyale.Source: Mwananchi

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments