SHARE

[ad_1]

Wachekeshaji Idris Sultan, Dogo Pepe, Captain Khalid, Chipukeezy wa Kenya na Salvado wa Kenya, Ijumaa hii walivunja mbavu za wapenzi wa stand up comedy jijini Dar es Salaam kwenye awamu ya tatu ya show ya Funny Fellas.

Idris Sultan
Sultan akiwa jukwaani kuonesha uwezo wake

Show hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa makumbusho ya taifa na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo mastaa. Mastaa waliohudhuria ni pamoja na Alikiba, Ommy Dimpoz, Navy Kenzo, Kajala, Queen Darleen, Feza Kessy na wengine.

Ali Kiba na Ommy Dimpoz
Alikiba na Ommy Dimpoz

Akiongea na Bongo5, Captain Khalid ambaye anashirikiana na Idris kuandaa show hiyo alisema muitikio wa watu umewapa nguvu zaidi na ana malengo ya kuifanya show hiyo kupanuka zaidi.
Amesema kwenye awamu inayokuja ya Funny Fellas July mwaka huu jijini Dar, Salvado atarejea tena na ataungana na mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi na Anne Kansiime wa Uganda watakuwepo.

Full furaha

“Funny Fellas basically ni mimi na Idris, ndio kama main resident halafu we have anybody,” amesema Captain Khalid. “Kwahiyo ni project ya mwaka mmoja tunaangalia itakuwaje ikishika mwaka ujao itakuwa kubwa zaidi.”

Kapteni Khalid
Captain Khalid

Navy Kenzo wakifuatilia show kwa makini
Navy Kenzo wakifuatilia show kwa makini

Amesema Funny Fellas imekuwa na mafanikio makubwa katika show zote tatu walizofanya. Amesema pamoja na comedy kuwa tasnia changa kwa Tanzania lakini inalipa. Kwa upande wake Chipukeezy wa Kenya ambaye umaarufu wake ulianzia kwenye kipindi cha Churchill Show, amesema stand up comedy inaweza kuwa kitu kikubwa iwapo Watanzania wataanza kwenda kwenye show za wachekeshaji wa nyumbani.

Mchekeshaji wa Kenya, Kipukiizy akifanya yake
Mchekeshaji wa Kenya, Chipukeezy

“Njia pekee ambayo itaweza kukua ni pale tutaweza kuwaunga mkono, kuwaunga mkono ni kwa kwenda. Hata wasanii wenyewe wana changamoto, usingoje miezi mitatu ndio ufanya show, pale Nairobi jamaa wanapiga show kila wiki hivyo inabidi wafanye show ili watu wawazoee,” alishauri Chipukeezy.

Dodo Pepe
Dogo Pepe

Kwa upande wake Dogo Pepe alisema bado stand up comedy ina changamoto Tanzania kwasababu kuna maeneo hata hawajui ni kitu.

Ice Boy kutoka High Table Sound
Rapper Ice Boy

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments

[ad_2]

Source link

Comments

comments