SHARE

[ad_1]

Kama unadhani Sam Misago amekurupuka kufanya rap baada ya kuwa amepata jina kwenye utangazaji wa redio na TV, uko wrong.

13181342_446989248914185_1668021518_n

Mtangazaji huyo wa East Africa TV na Radio ameiambia Bongo5 kuwa rap ndiyo iliyompa kazi ya kwanza ya redio. “Watu hawafahamu kwamba before mimi nimekuwa kwenye redio nilikuwa rapper na nilivyopeleka wimbo wangu kwenye redio zamani Triple A ndio Sophia Kessy akaisikia sauti yangu akaniambia unapendezea kinoma ukiwa mtangazaji na ndio Sophia Kessy akanipa kazi, Sophia ambaye kwa sasa yupo Clouds,” amesema Sam.

“Nilivyoanza utangazaji nikajikuta napenda kinoma kutangaza so ikachukua sehemu kubwa kinoma ya maisha yangu, kutangaza kwenye redio na kutangaza kwenye TV so mwisho wa siku nikasahau kabisa mambo ya kufanya muziki. Na pia niligundua kuwa ni career ambayo ina heshima kubwa,” amesisitiza.

Sam amedai kuwa maoni hasi anayoyapata kutoka kwa baadhi ya watu kuhusu muziki wake hayamkatishi tamaa zaidi ya kumpa nguvu ya kukaza zaidi.

Amesema bado ataendelea kufanya muziki na hivi karibuni atakuja na ngoma mpya

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments