SHARE

[ad_1]

Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 25, 2016 inaingia tena katika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa India kukipiga na Malaysia katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kwenye michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

serengeti-new

Katika mchezo wa kuwania kucheza fainali, Serengeti Boys iliruhusu sare ya mabao 2-2 Malaysia hivyo kufikisha sare ya tatu baada ya kushinda mechi moja. Serengeti Boys imemaliza hatua ya awali ikiwa na pointi sita sawa na Korea Kusini, lakini ikazidiwa bao moja hivyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ambayo Marekani iliongoza kwa kufikisha point nane.

Licha ya kuwa wenyeji, India ilitupwa mbali hivyo kwa kesho watakuwa watazamaji katika michezo yote miwili ukianzia wa Serengeti Boys na Malaysia utakaopigwa saa 7.30 mchana kwa saa za Tanzania kabla ya fainali kuchezwa saa 11.30 jioni kati ya Marekani na Korea Kusini.

India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments