SHARE

[ad_1]

Inasikitisha kilichotokea mitandaoni kwa dada zangu wawili ninaowaheshimu sana kwenye muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammedi aka Shilole na Vanessa Mdee aka Vee Money.

Shishi

Usiku wa Jumanne ulikuwa ni wa furaha kwa wale wasiopenda maendeleo kwani walitumia msemo “vita vya panzi furaha ya kunguru” baada ya Shilole na Vanessa kutupiana maneno ya kukashifiana na kutishiana wakati kila mmoja akijua dhahiri hilo ni kosa kisheria.

“Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliandika Shilole.

Vanessa alijibu kwa kuandika: “ Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent.”

Sitaki kuamini kuwa kilichokuwa kimefanyika ni kutafuta kiki kwa wanadada hao ya wimbo ‘Say My Name’ wa Shilole na kuandaa mazingira ya albamu mpya ya Vanessa ‘Money Monday’ ambayo amepanga kuiachia mwaka huu japo muda haujajulikana.

Shilole alimuonya Vanessa kwa kupost kipande cha video kilichokuwa na baaddi ya maneno yaliyosema, “Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol.”

Funika kombe mwanaharamu apite, lakini Vanessa hakutaka kujua hilo alijibu mapigo kwa kutuma kipande cha video na yeye kwa kusema, “But look, there is now way, there is no time, it’s too much effort to try lower a little myself and what I stand for your nonsense, kama huelewi chukua time na vimaneno vyako viwili vya Kiingereza.”

Kwanini hiyo nguvu ya kutishiana na kutupiana maneno ya kejeli mitandaoni msingetumia kutafuta vipaji vya wasanii wengine wa kike wakati munajua wasanii wa kike bongo mpo wachache na mnao kick hamzidi watano?

Vanessa unaonekana umetoboa Afrika nategemea kuona makubwa kwako lakini kwa hiki kilichotokea umeniangusha. Napenda kusikiliza nyimbo yako ya ‘Hawajui’ kwanini usijifunze kutokana na mashairi yako uje kuwa Queen of Africa kutokea bongo.

Napenda kuona tena Shilole na Vanessa wakipeana support kwenye vitu vya maana na kushikana mikono kuupanua muziki wetu kwa kuwaonyesha watu wa nje kuwa bongo tuna wasanii wa kike pia wanaofanya vizuri siyo kina Alikiba, Diamond, AY, Joh Makini pekee.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments

[ad_2]

Source link

Comments

comments