SHARE

[ad_1]

Kundi la akina dada lililowahi kutamba duniani, Spice Girls linaungana tena. Member watatu kati ya watano wameingia studio kutengeneza kazi mpya.

1997_spice-girls-8_2259097k

Geri Horner (Ginger Spice), Melanie Brown (Scary Spice) na Emma Bunton (Baby Spice) walitumia saa 40 kwenye studio za Play Deep jijini London kurekodi nyimbo mpya huku wakipanga kuachia album mpya baadaye mwaka huu kusherehekea miaka 20 tangu watoe album yao ya kwanza, Wannabe.

Pia mwaka 2017 watafanya show za live katika maeneo mbalimbali. Jumatano hii Mel B alipost picha Instagram akiwa na wenzake hao wawili na kuandika, “And I say oohhhh LALA.”

13099054_890686351057315_1590581005_n

Hata hivyo Victoria Beckham (Posh Spice) hatohusika huku pia Mel C (Sporty Spice) hakuwepo kwenye studio za Play Deep baada ya mapema mwaka huu kudai kuwa atafanya muziki mwenyewe.

Wamewahi kuungana tena kwa muda mfupi mwaka 2007 na 2012.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments