SHARE

Mwanamziki Amani amechoshwa na maswali kutoka kwa wanahabari na mashabiki wake wakitaka kujua iwapo ni ‘mjamzito’

Mashabiki wa Amani wamekuwa wakiulizia iwapo mwimbaji huyo ana mimba. Mwimbaji huyo sasa anataka tetesi hizo zikome.

 

0fgjhs31h9h0slm4b.b3709a3a

Mwimbaji Amani

 “ Hii ndiyo mara ya mwisho ninayojibu swali hili ambalo huniudhi sana kila linapoulizwa,” Amani alisema katika mahojiano na SDE baada ya tetesi kuibuka katika mitandao jamii kuwa alikuwa mjamzito. “ Nataka kusema bayana kuwa mimi si mjamzito kama walivyosema baadhi ya wasabasi ambao wana kipawa cha kujua iwapo mwanamke ni mja mzito kwa kumuangalia,”

Mwanamziki huyo aliye na umri wa miaka 35 alitumbuiza katika tamasha la ‘Plot’  Ngong  Agosti 13 2016 alipoungana na msanii wa Marekani Ginuwine na Mya.

Akijibu swali hilo lililoulizwa na mwandishi wa gazeti moja maarufu nchini, Amani alisema:

 “ Ooh! Nashangaa kusikia hilo kutoka kwako,” alisema.
0fgjhsoqguftttl34.fe7ea245

Amani akitumbuiza tamasha la ‘Plot’ mnamo Agosti 13 2016.

“ Lazima una kipaji cha hali ya juu kama unaweza kujua mwanamke mjazito kwa kumuangalia. Mimi si mjamzito” alisema.

Mwimbaji huyo yuko katika uhusiano ijapokuwa hakufafanua zaidi.

Comments

comments