SHARE

[ad_1]

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Young Killer Msodoki amesema sio kitu rahisi kufanya kazi na Mr Blue ambaye alikuwa akisikiliza kazi zake wakati yupo shuleni.
kumekucha

Rappa huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo ‘Kumekucha’ akiwa amemshirikisha Mr Blue, ameiambia Bongo5 kuwa kufanya kazi na mkali huyo wa wimbo ‘Pesa’ ni kuendelea kuandika historia ya muziki katika maisha yake.

“Kusema kweli Mr Blue ni msanii ambaye nilikuwa namsikiliza wakati nikiwa dogo sana, yaani wakati nipo shule, mashairi naandika kwenye daftari,” alisema Young Killer.

“Nimeanza kukutana naye kwa Mona studio, akawa ananisifia huyu dogo mkali sana, kaza, Kwenye matamasha, Sasa leo nimefanya naye ngoma huku ni kuandika historia, kwa sababu siyo kitu rahisi, aliangalia uwezo wangu ndio maana akakubali kufanya na mimi,” Aliongeza.

Young Killer amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya video ya wimbo huyo ambayo ataiachiwa wiki ijayo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments


[ad_2]

Source link

Comments

comments